Taarifa inatolewa kwamba mkutano mkuu wa pili wa wanahisa wa Yetu Microfinance Bank PLC utafanyika siku ya jumamosi tarehe 10 Juni, 2017 katika ukumbi wa msimbazi Dar es Salaam kuanzia saa tano(5:00) kamili asubuhi kujadili dongoo zifuatazo.
- Kufungua Mkutano
- Kuridhia dondoo
- Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano wa kwanza
- Kujadili yatokanayo na kumbukukumbu za mkutano wa kwanza
- Kupokea na kujadili taarifa za bodi ya wakurugenzi na taarifa za hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2016.
- Taarifa ya bodi ya wakurugenzi
- Hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2016
- Gawiwo kwa mwaka 2016
- Kuidhinisha ada ya wakurugenzi
- Kuteua wakaguzi wa hesabu
- Menginayo kwa idhini ya mwenyekiti
- Kufunga mkutano
MAELEZO:
- Makabrasha ya mkutano yanapatikana matawini na kwenye vituo vyetu kuanzia tarehe 2 Juni, 2017,vinginevyo yatapotikana kwenye ukumbi wa mkutano tarehe 10 Juni, 2018.
- Wanahisa wanaotaka kuhudhuria mkutano, watajigharamia usafiri na malazi na hapatakuwa na malipo ya posho
TAARIFA YA SEMINA KWA WANAHISA
Kutakuwa na semina kwa wanahisa itakayolenga kutoa elimu ya “Fursa na Changamoto za uwekezaji katika hisa”, taratibu mbali mbali mwanahisa anatakiwa kuzifahamu kuhusu uwekezaji wake, taaratibu za uuzaji wa hisa na vitu vinavyoathiri thamani na bei ya hisa katika soko. Semina hio itafanyika siku ya mkutano kuanzia saa mbili na nusu hadi saa tano katika ukumbi wa msimbazi centre.