Mkutano wa kwanza wa wanahisa
TAARIFA INATOLEWA KWAMBA, Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanahisa wa Yetu Microfinance Bank Plc utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 24 Septemba, 2016 katika Ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi.
Agenda
- Kuridhia Agenda za Mkutano.
- Kuchagua na kuthibitisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
- Mengineyo
Maelezo
- Mwanahisa atakayehudhuria Mkutano Mkuu atatakiwa kujigharamia mwenyewe na aje na Hati ya Hisa iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam pamoja na kitambulisho chake,kadi ya kupiga kuira au hati ya kusafiria au kitambulisho cha kazi. Fomu ya mwakilishi mbadala(proxy form) itapatikana ofisi za YETU,makao makuu zilizopo Jengo la Mkunazini, ghorofa ya 2,mtaa wa Kiungani-Kidongo Chekundu na matawi yote na ofisi za madalali wa Soko la Hisa Dar es Salaam kuanzia tarehe 9 Septemba,2016.
- Mwanahisa anayestahili kuhudhuria na kupiga kura lakini akashindwa kuhudhuria kikao,anaweza kuwasilisha Jina la mbadala wake(proxy) kwa Katibu wa Bodi katika ofisi za YETU makao makuu zilizopo jengo la Mkunazini, ghorofa ya 2,mtaa wa Kiungani-Kidongo chekundu au kwenye kikao. Kwa makampuni, fomu inapaswa kuwa katika lakiri ya kampuni mwanahisa.
- Ili kujua wanahisa wanaostahili kupiga kura ,Rejesta ya Wanahisa itafungwa Jumatano tarehe 21 Septemba,2016.
TAARIFA YA SEMINA KWA WANAHISA
Taarifa inatolewa kwamba kutakuwa na semina kwa Wanahisa itakayolenga kutoa elimu kuhusu “Jinsi Wawekezaji Wanavyoweza Kutumia Fursa za Uwekezaji Katika Soko la Hisa” Semina hiyo itafanyika Ijumaa, tarehe 23 Septemba,2016 katika ukumbi wa Msimbazi Centre, kuanzia saa 3.00 asubuhi.
KWA IDHINI YA BODI
Joyceline Kobero
Katibu wa Benki
Septemba , 2016