Nafasi ya ujumbe wa bodi
Yetu Microfinance Bank inatangaza nafasi ya ujumbe wa Bodi na kukaribishaa maombi kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo.
MAJUKUMU
- Kusimamia dira na dhima ya benki
- Kuandaa,kusimamia na kutathimini sera na mikakati ya benki
- Kupitia na kurejea mara kwa mara sera na miongozo ya Benki zikiwemo sheria za nchi
- Kushiriki katika uteuzi na usimamizi wa kazi za mtendaji Mkuu wa benki
- Kutathmini utendaji wa Bodi,mmoja mmoja na kwa ujumla
- Kushiriki vikao vya Bodi,Kamati na mikutano muhimu
- Kutimiza jukumu la uwajibikaji kwa wanahisa
- Majukumu mengine kama yanavyoainishwa na sheria
SIFA ZA MGOMBEA
- Awe ni mwanahisa
- Awe na elimu kuanzia ngazi ya stashahada na kuendelea na uzoefu katika sekta ya benki kwa muda usiopungua miaka mitano
- Umri usiozidi miaka 67
- Asiwe na rekodi ya kesi ya jinai au kufilisiwa
Maombi yatumwe kwa
Mkurugenzi Mtendaji
Yetu Microfinance Bank PLC
P.O.Box 75379
Jengo la Mkunazini, Ghorofa ya 2,Mtaa wa Kiungani-Kidongo Chekundu
Dar es Salaam
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 16.09.2016