TAARIFA KWA UMMA
KUONGEZA MUDA WA TOLEO LA HISA ZA YETU MICROFINANCE PLC
Tunafurahi kuwatangazia wawekezaji na wadau wa sekta hii kuwa muda wa kuuza hisa za Yetu Microfinance PLC umeongezwa hadi tarehe 29 Agosti 2015. Ili muweze kufaidika na uwekezaji katika Kampuni hii inayoshughulika na huduma za kibenki kwa wajasiriamali na biashara ndondogo, mnakaribishwa kununua hisa zenu kwa wakala wafutao:
- Makao makuu ya Yetu Microfinance na matawi yake Dar es Salaam na quality centre;
- Matawi ya Yetu Microfinance – Ifakara, Kilwa, Mngeta na Zanzibar;
- Madalali wote wa Soko la Hisa la Dar es Salaam;
- Matawi yote ya Benki ya CRDB, benki mkusanyaji mkuu;
- Matawi yote ya mabenki makusanyaji yafuatayo:
- Benki ya Posta;
- Benki ya Mkombozi;
- Benki ya Akiba Commercial Bank;
- Benki ya Wanawake Tanzania;
- Benki ya Azania Bancorp;
- Mbinga Community Bank;
- Mufindi Community Bank;
- Meru Community Bank;
- Njombe Community Bank;
- Kagera Farmers’ Cooperative Bank;
- Kilimanjaro Cooperative Bank.
Tafadhali fika na kitambulisho chako na fedha taslimu.